Home » Articles » WORKSHEET » Upper Primary

KISWAHILI CODE: KISW160001

JARIBIO:
KISWAHILI

KIWANGO:
ELIMU YA MSINGI JUU

KODI:
KISW160001

JUMLA YA MASWALI:
25


1. Mwanafunzi huyu akisoma kwa bidii ___________ mtihani wake.
A. akifaulu B. atafaulu C. anafaulu D. angefaulu E. alifaulu

2. Binti mrembo ni ndugu yangu. Katika sentensi hii kuna jumla ya vivumishi vingapi?
A. Kimoja B. Vitatu C. Viwili D. Vitano E. Vinne

3. Neno mapambazuko ni kisawe cha neno lipi kati ya haya?
A. Machweo B. Magharibi C. Mapamba D. Mawio E. Kumekucha

4. Wanafunzi wema waliniletea zawadi nzuri. Kiambishi ‘ni’ katika neno waliniletea kinawakilisha nini?
A. Kiambishi cha kati cha nafsi ya tatu mtenda
B. Kiambishi awali cha nafsi ya tatu mtendewa
C. Kiambishi awali cha nafsi ya kwanza mtenda
D. Kiambishi tamati cha nafsi ya kwanza mtendewa
E. Kiambishi awali cha nafsi ya kwanza mtendewa

5. Ng’ombe wao wanatoa maziwa mengi kuliko ng’ombe wetu. Andika umoja wa sentensi hii.
A. Ng’ombe wake anatoa maziwa mengi kuliko ng’ombe wangu
B. Ng’ombe wao anatoa maziwa mengi kuliko ng’ombe wetu
C. Ng’ombe wake wanatoa maziwa mengi kuliko ng’ombe wangu
D. Ng’ombe wake anatoa maziwa machache kuliko ng’ombe wangu
E. Ng’ombe wao hatoi maziwa mengi

6. Lango lile li wazi. Neno ‘li’ kama lilivyotumika katika sentensi linasimama kama aina gani ya maneno?
A. Kiunganishi B. Kihisishi C. Kitenzi D. Kiingizi E. Kiwakilishi

7. Neno ambalo ni tofauti kati ya haya ni ___________
A. Ngalawa B. Meli C. mkokoteni D. mtumbwi E. mashua

8. Hivi _________ alivyo rafiki yetu Zuwena.
A. ndiye B. ndivyo C. vyote D. ndio E. ndio

9. Kijana Salai alikuwa mwizi, lakini ______ siku nyingi akakamatwa.
A. haikupita B. haukupita C. hakupita D. hazikupita E. haitapita

10. Andika mchanganuo wa sentensi hii.
Wanafunzi huamka asubuhi na mapema sembuse ninyi?
A. N + Ts + N + N + U
B. W + t + E + t + W
C. N + t + N + N + t + W
D. N + t + N + Ts + W
E. N + T + E + U + W

11. Kuna aina ngapi za silabi katika neno kindumbwendumbwe?
A. Tatu B. Tano C. Kumi na moja D. Mbili E.Hakuna jibu

12. Nomino ipi ambayo haikuambatana na ngeli yake swadakta?
A. Mti > U – i
B. Muwa > U – i
C. Miba > U – i
D. Ugonjwa > U – I
E. Mwamba > U – i

13. Katika neno wananirukia, viambishi awali ni __________
A. wana B. wa C. wanani D. wananir E. a

14. Kinyume cha neno kinai ni _____________
A. chosha B. kaditama C. penda D. hamu E. kinaishwa

15. Angesoma angefaulu. Neno nge hubainisha ___________
A. hali tegemezi B. hali timilifu C. hali mazoea
D. hali masharti E. hali isiyodhihirika

16. Mwanafunzi amefundisha badala ya mwalimu wake. Hii ni aina gani ya sentensi?
A. Shurutia B. Ambatano C. Tegemezi D. Changamano E. Sahili

17. “ Niletee daftari lako mwalimu alisema”. Kauli taarifa ya sentensi hii ni _______
A. Mwalimu alisema kuwa nimletee daftari langu
B. Mwalimu alisema kuwa nilete daftari
C. Mwalimu alisema kuwa anahitaji daftari langu
D. Mwalimu alisema kuwa nimpelekee daftari langu
E. Mwalimu alisema kwamba nimpelekee lile daftari

18. Chakula _________ kuanzia kinywani hadi tumboni.
A. humegeka B. hutafunwa C. husagika D. humwagika E. humeng’enywa

19. Sababu ya neno ukweli kuwa katika ngeli ya U – U ni _____________
A. neno ukweli huanza na irabu u
B. neno ukweli halina mabadiliko katika umoja na uwingi
C. neno ukweli lina kiambishi awali cha u
D. neno ukweli ni nomino dhaharia
E. neno ukweli kinyume chake ni uongo

20. Kiambishi kinachoonesha njeo katika neno hufyeka ni _________________
A. – fye - B. – ka - C. hu - D. a E. – fyek –

SEHEMU B: MSAMIATI

21. Ng’ombe dume aliyehasiwa huitwa maksai, binadamu aliyehasiwa huitwa______
A. mgumba B. tasa C. towasha D. towashi E. mwanamwali

22. Ng’ombe jike ambaye bado hajazaa huitwa ________
A. mbuguma B. ndama C. fahali D. maksai E. mori

23. Mtu anayekuingia moyoni na kukuthamini kuliko mtu mwingine huitwa ________
A. mahabuba B. rafiki C. swaiba D. mahabubu E. shoga

24. Jogoo ambaye hajaanza kuwika hujulikana kama ___________
A. jimbi B. pora C. kijimbi D. kifaranga E. kijogoo

25. Mtunzi wa mashairi hujulikana kama malenga. Je mwimbaji wa taarabu huitwa _
A. Manju B. mghani C. mutribu D. mshereheshaji E. mwanamipasho

BOFYA HAPA KUANGALIA MAJIBU YOTE

THE ANSWERS ARE:

1 B
2 C
3 D
4 E
5 A
6 C
7 C
8 B
9 D
10 E
11 B
12 D
13 C
14 D
15 D
16 E
17 D
18 E
19 B
20 C
21 B
22 E
23 D
24 B
25 C
Category: Upper Primary | Added by: Admin (02/Jul/2017) | Author: Yahya Mohamed E W
Views: 255 | Tags: KISW160001 | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: