Home » Articles » HEALTH

SABABU NA ATHARI ZA MADAWA YA KULEVYA

MADAWA YA KULEVYA


Madawa ya kulevya ni vitu ambavyo hutumiwa kwa njia ya kunywa, kula au hata kujichoma ambavyo baada ya kutumia hubadili akili au fikra za mtumiaji kuwa tofauti ba akili ya kawaida. Madawa haya hayatumiwi kwa lengo la kuleta tiba au manufaa katika mwili bali hutumiwa kwa lengo la kujistarehesha tu. Mfano wa madawa ya kulevya ni kama vile bangi, mirungi, pombe, cocaine na kadhalika.

Kuna mambo mbalimbali ambayo humfanya mtu kujiingiza katika tabia hii ya utumiaji wa madawa ya kulevya kama ifuatavyo:-

Marafiki wenye vishawishi vibaya: kujiunga na marafiki ambao ni watumiaji wa madawa ya kulevya husababisha ushawishi mkubwa sana wa mtu naye kujiung ana nao kwani wahenga walisema ndege wenye manyoya ya kufanana hutembea pamoja.

Hali ngumu ya maisha kutokana na sababu mbalimbali pia huweza kuwa ni sababu ya mtu kujiunga na utumiaji wa madawa ya kulevya na hatimaye naye kuwa mtumiaji mkuu kwa mfano, wale wanaosafirishwa nchi za nje kwa lengo la kuuza na kujipatia kipato mara nyingi huanza kuonja na hatimaye kuwa watumiaji wa kudumu. Mfano wa madaw ahayo ni cocaine.

Kukosa udhibiti katika umri wa kubalehe au kuvunja ungo kwa wasichana, kipindi hiki vijana hujiingiza katika kala aina ya tabia mbaya na humu wengine huanza kutumia madawa ya kulevya kama vile uvutaji wa bangi, unywaji wa pombe utumiaji wa cocaine na mengineyo, hivyo kijana akikosa udhibiti kutoka kwa wale wanaomlea humfanya aanze na hatimaye kudumu na tabia hizi.

Kuchanganyika kwa mila na desturi za ndani na nje ya nchi. Hii hutokana na wahamiaji kutoka nje ya nchi ambazo sera na sheria zao ni tofauti na za nyumbani mfano nchi kama Kenya utumiaji wa mirungi ni halali wakati Tanzania sio halali hivyo wanapokuja kutoka Kenya kuja Tanzania huja na mazoea ya nyumbani kwao hivyo huambukiza hadi wenyeji wanaowakuta nao kujiingiza katika utumiaji wa vitu hivyo.

Kuwa na msongo wa mawazo kutokana na sababu mbalimbali humfanya mtu atumie madawa ya kulevya  kwa kuamini kwamba akitumia ataliwazikana kusahahu matatizo yote aliyonayo mfano matatizo ya kifamilia, ya kikazi, ya ndoa na mengineyo.

Hizo ndizo sababu zinazoweza kumfanya mtu ajiingize katika matumizi ya madawa ya kulevya, na kuna hasara mbalimbali ambazo mtu huweza kuzipata au hata jamii kwa ujumla kama ifuatavyo:-

Maambukizi ya magonjwa mbalimbali kama vile UKIMWI, saratani na kadhalika. Yapo madawa ambayo husababisha saratani ya mapafu, mifupa na damu kama vile bangi na mengine husababisha kijana kujihusisha na makosa ya jinai kama vile ubakaji na hatimaye kuambukizwa UKIMWI.

Kupungikiwa na nguvu kazi ya taifa. Wengi wanaotumia madawa ya kulevya hushindwa kufanya kazi zinazoleta maendeleo katika jamii na kuwa kama mizigi isiyobebeka katika jamii na wengine hufa katika umri mdogo kutokana na maradhi ya kuambukizwa.

Ujauzito katika umri mdogo na kusababisha watoto wa mitaani kujaa katika jamii. Hii hutokana na wasichana watumiao madawa ya kulevya kushirikiana na wavulana watumiao madawa ya kulevya na kujenga uhusiano na hatimaye kupata ujauzito, hali hii hufanya watoto wa mitaani kujaa katika jamii kwani hukosa malezi kutoka kwa wazazi wao pengine wameshakufa au kutokuwa na uwezo wa kuwalea kwasababu ya tabia hii ya utumiaji wa madawa ya kulevya.

Uhalifu na uharibifu wa mali katika jamii. Watu wanaotumia madawa ya kulevya mara nyingi sana hawana uwezo wa kujikimu kimaisha hivyo hutumia mbinu mbalimbali ili wapate kipato japo kidogo tu kwaajili ya kununulia madawa ya kulevya na chakula mfano ukabaji, uporaji na kadhalika hivyo amani katika jamii hutoweka na mali za wanajamii kupotea.

Athari nyingine ni kupata matatizo ya kimaumbile kama vile ukosefu wa uzazi, kukosa nguvu za kiume, upofu na kuvurugika kwa mfumo wa sauti, mfano mirungi hukosesha nguvu za kiume na bangi huvuruga au huweza kuharibu baadhi ya mishipa ya fahamu na kusababisha upofu na matatizo mengineyo.

Hizo ni athari zinazoweza kusababishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya, hivyo basi ni vema tuelimishane juu ya madhara ya kutumia madawa haya na tulindane na tulee vijana wetu katika maadili yaliyo bora kabisa na kuchukulia hatua kali kabisa wale watakaojulikana wanajihusisha na uuzaji au utumiaji wa madawa ya kulevya.

Sina mengi juu ya hayo, ikiwa una maoni au ushauri au maswali jisikie huru kuuliza hapa. Tuko kwaajili ya kuelimisha jamii. Ahsante.

Category: HEALTH | Added by: Admin (10/Oct/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 3366 | Rating: 2.0/1
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: