Home » Articles » HEALTH

Nini maana ya Kufeli au kufa kwa moyo? (Heart failure) Na nini kisababishi?

Nini maana ya Kufeli au kufa kwa moyo? (Heart failure) Na nini kisababishi?

 

Ingawa inaweza kuleta maana hiyo Lakini kufa kwa moyo haina maana kwamba moyo umeshindwa kufanya kazi au umefeli. Kufeli kwa moyo ni hali mbaya sana ambayo moyo hausukumi damu ipasavyo katika mwili. Upande wa kulia wa mgonjwa au kushoto au hata kotekote kunaweza kuathirika. Dalili zake hutegemea ni upande upi umeathirika na ni kwa kiasi gani kufeli kwa moyo kumejitokeza.

Kutokana na baadhi ya wataalamu wa mambo ya moyo wameweza kueleza kwamba  kufeli kwa moyo ni "ukosefu wa kazi hii ya kusuma damu vizuri katika mwili, hivyo pampu zinashindwa kuzungusha damu mwilini na matokeo yake kuw ana msongamano mkubwa sana katika tishu (tissue).


Idadi ya wazee wenye matatizo haya wanazidi kuongezeka hasa hasa katika nchi zenye viwanda na maendeleo, hasa hasa marekani. Vilevile tatizo hili limekuwa ni sababu inayoongoza ya vifo kusini na mashariki mwa bara la Asia.


Takriban nusu ya wagonjwa wa tatizo hili wana matatizo ya kumbukumbu, yaani hupoteza kumbukumbu na pia katika mtazamo wa utambuzi, hii ni kutokana na mtafiti kutoka chuo kikuu cha California, Davis.

Kuna aina kama tatu hivi za matatizo ya moyo ambayo watu wengi sasa huchanganya au hushindwa kutofautisha, nayo ni Heart Failure, Heart Attach na Cardiac Arrest. Hebu tuangalie tofauti za matatizo haya.

 1. Heart attack – hii hutokana na kuharibika au kufa kwa misuli ya moyo kwa kule kuziba kwa mishipa au ateri za moyo (coronary artery). Tishu za misuli ya moyo hufa kwasababu ya kukosa oxygen (kwasababu damu haingii humo).
 1. Heart failure – hii ina maana misuli ya moyo haiwezi kusukuma damu mwilini ipasavyo. Hii siyo heart attack.
 1. Cardiac arrest – hii ina maana mapigo ya moyo husimama kabisa, moyo husimama, mzunguko wa damu husimama, moyo haudundi kabisa.

Kwa kufupisha ni kwamba Heart attack ina maana seli za moyo hufa kutokana na kukosa oxygen, Heart failure ina maana moyo hausukumi damu ipasavyo na Cardiac arrest ni moyo kusimama kabisa.

Je, nini alama au daliliza tatizo hili? (Heart Failure)

Unashauriwa kumuona mtaalamu wa moyo haraka sana endapo utaona una dalili hizi.

 • Kuzunguzungu kikali – hii husababisha pia kuchoka sana, mgonjwa anakuwa hapati damu ya kutosha katika misuli yake.

Dalili zingine hutegemea ni upande gani umeathirika

 • Kufeli kwa moyo upande wa kushoto

1.       Upungufu wa pumzi, kutweta – hii huweza kutokea muda wowote, Lakini huweza kugundulika kwa urahisi zaidi endapo mgonjwa atakuwa amelala au kujishughulisha. Mgonjwa usiku atakuwa anahitaji kukaa badala ya kulala ili apate hewa nyingi iliyo safi.

2.       Kukohoa

3.       Kutoa mapovu wakati wa kukohoa

Hii hutokea pale damu inaporudi katika vena za pulmonary, kwasababu moyo umeshindwa kuendelea kusukuma damu hivyo kusababisha kimiminika kuingia katika mapafu

 • Kufeli kwa moyo upande wa kulia

1.    Kuvimba kwa visukusuku vya miguu na mikono

2.    Kuvimba miguu

3.    Kutanuka kwa ini

4.    Kuvimba tumbo

Hali hii hutokea pale damu inapotoka kwenye moyo inapopungua kasi, hivyo damu inayorudi katika moyo kupitia mishipa hurudi, na kusababisha kujaa kwa kimiminika katika tishu. Figo hupata shida sana kuchuja maji na chumvi ambayo husababisha upungufu wa kimiminika katika tishu.

 

 • Kufeli kwa moyo pande zote mbili.

1.    Kizunguzungu – jinsi kiasi cha sodium na vitu vingine katika damu vinapobadilika ndipo mgonjwa hupata uwezekano mkubwa sana wa kuhisi kizunguzungu na kuchanganyikiwa.

2.    Kichefuchefu

3.    Kufunga choo (constipation)

4.    Kukosa hamu ya kula – pindi mfumo wa mmeng’enyo unapopokea damu chache, ndipo mgonjwa huhisi kukosa hamu ya kula na matatizo ya mfumo wa mmeng’enyo.

Tumeona dalili za kufahamu kama una tatizo la kufeli kwa moyo sasa hebu tuangalie ni vitu gani ambavyo vinavyosababisha tatizo hili?

Zifuatazo ndiyo sababu:

 • Kisukari – hasa kisukari type 2 (huwa vina aina zake)

 • Unene uliopita kiasi – watu wenye unene uliopita kiasi na hali ya kuwa wana kisukari type 2 kama tulivyozungumza hapo juu basi wana hatari ya kupata tatizo hili mara mbili zaidi.

 • Uvutaji wa sigara – watu wanaovuta sigara na wanaodumu na hali hii huwa na asilimia kubwa ya uwezekano wa kupata tatizo hili la kufeli kwa moyo.

 • Presha ya kupanda (Hypertension)

 • Kuwa na sababu zote hizi nne- kisukari, uzito uliozidi, uvutaji wa sigara na presha ya kupanda wamewekwa katika kundi la wenye kupata tatizo hili hasahasa kwa kuathirika upande wa kushoto kwa kipindi kifupi sana takriban miaka minne (4)au kwa wingi kumi na sita (16).

 • Ukubwa wa kiuno – imegundulika kuwa ukubwa wa kiuno umekuwa ni sababu ya tatizo hili kwa watu wa umri wa kati na wazee, na imegundulika kwamba ni hatari hata kama uzito wa mtu huyu uko sawasawa.

 • Heart Attack (coronary heart disease).

 • Msongo wa mawazo hasahasa kwa wale wenye matatizo ya moyo.

 • Magonjwa ya moyo ya kurithi.

 • Anaemia – upungufu wa damu au seli nyekundu za damu.

·         Hyperthyroidism (kupitiliza au kuzidi kwa tezi za thyroid).

 

·         Hypothyroidism (kupunguza kwa tezi za thyroid).

 

·         Kufeli kwa moyo upande wa kushoto kunaweza kusababisha kufeli upande wa kulia.

 

·         Kuharibika kwa valvu za moyo.

 

Kwa upande wangu nina hayo tu, ikiwa una la ziada itakuwa ni bora tukachangia mada kwa lengo la kuelimisha jamii na kutatua matatizo. Jisikie huru katika mtandao huu wa Staryte – The informative where we get what we find. Ahsante.

Category: HEALTH | Added by: Admin (19/Sep/2013)
Views: 2554 | Rating: 2.0/2
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: