Home » Articles » EDUCATION

UKWELI KUHUSU NYOKA MWENYE VICHWA VIWILI

UKWELI KUHUSU NYOKA MWENYE VICHWA VIWILI

Je, Nyoka hawa wapo au ni hadithi tu?Ukweli ni kwamba nyoka mwenye vichwa viwili yupo, lakini ni wachache sana. Hawa nyoka ni kama mapacha walioungana au unaweza kusema kuwa ni nyoka mmoja mzima lakini ana vichwa viwili vilivyokaa mbadala yaani nyuma na mbele. Nyoka hawa sana sana unaweza kuwaona katika mbuga za wanyama au sehemu za kutembelea kiutalii zenye maonyesho ya wanyama wa aina mbalimbali. Baadhi ya sehemu za makumbusho wamehifadhi masalia au sampuli ya nyoka hawa wenye vichwa viwili.

Nyoka wenye vichwa viwili hawana matarajio ya kuishi muda mrefu, hasa hasa porini. Kila kichwa kina ubongo na siku zote vinaendesha mwili mmoja, na vichwa hivyo viwili haviwezi kuwasiliana hali ambayo husababisha kujongea kwa tabu kwani kila kichwa kinaweza kujaribu kutembea kulekea muelekeo tofauti mpaka pale kimoja kitakapokubali kuacha mvutano huu na kuvutwa na mwenzake. Na jambo ambalo ni baya zaidi ni pale kila kichwa kinapotaka kula ingawa mwili ni mmoja hivyo hukuta katika mazingira ya kugombania chakula.

Baadhi ya nyoka wenye vichwa viwili huchangia tumbo moja, wakati wengine huwa na tumbo kwa kila kichwa. Kwa wale wenye matumbo tofauti kuna hatari zaidi ya kufa kichwa kimoja kwa kukosa chakula endapo watakua wakigombania, lakini wanaochangia tumbo moja hawana neno kwani hata kimoja kikikosa chakula lakini kwa kuwa njia ya kuhifadhia chakula ni moja hivyo maisha yao kuendelea ingawa tatizo nalo pia kwa hawa huweza kutokea kwa  kukosa chakula pale wanapogombania windo lao na kusababisha windo hilo kukimbia.

Ingawa kuna magumu haya yanayowakuta nyoka hawa, lakini baadhi ya nyoka wenye vichwa viwili wamejulikana kuishi kwa takriban miaka 20 tangu walipokamatwa na kuhifadhiwa sehemu ya maalum. Thelma and Louise, nyoka mwenye vichwa viwili ambaye aliishi katika mbuga ya San Diego huko California, alikuwa na watoto 15 katika maisha yake. Watafiti wametoa nadharia kwamba uzao wa nyoka wa aina moja hii  kwaajili ya  mbuga unaweza kuongeza mategemeo ya nyoka wenye vichwa viwili, lakini hili ni gumu sana, kama haliwezekani kuthibitisha mpaka kulazimika kupata ujuzi juu ya jinsi gani nyoka hawa wanazaliwa huko porini. Uhakika wa kwamba wanaweza wasiishi muda mrefu inafanya kazi hii pia kukatisha tamaa.

Mnamo mwaka 2000, nyoka mwenye vichwa viwili aliyepewa jina la "We” aliwekewa oda ya dola laki moja na nusu ($150,000) sawa na Shilingi milioni mia mbili na arobaini za kitanzania kwa sasa (240,000,000/=) katika mtandao wa biashara eBay. Lakini kutokana na kanuni za mauzo katika mtandao huu kuhusiana na wanyama wanaoishi, mauzo haya hayakukubaliwa. Badala yake shirika la Nutra Pharma walimpata nyoka huyu mwaka 2006 ili asaidie katika masomo yao yanayohusu faida za kitaaluma ya madawa za sumu ya nyoka.

Jisikie huru kuuliza maswali, ushauri na maoni katika kisanduku hapo chini.


Category: EDUCATION | Added by: Admin (08/May/2013)
Views: 1841 | Tags: nyoka, viwili, chakula, sumu, ukweli, vichwa | Rating: 2.3/3
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: