Home » Articles » EDUCATION

SIRI YA KINYONGA NA KUBADILISHA RANGI YAKE

SIRI YA KINYONGA NA KUBADILISHA RANGI YAKE

Kinyonga ni kiumbe aliye katika kikundi cha mijusi (mfano: Mamba, Kenge, mjusi mwenyewe) ambaye ana uwezo wa kubadilisha rangi yake na kuzungusha macho yake kwa mizunguko tofauti, tofauti na wanyama wengine kwamba macho huzunguka kwa kufuatana, Lakini kinyonga na uwezo wa kuzungusha kila jicho upande wake.

Kinyonga habadilishi rangi kwa hiari yake, tofauti na watu wanavyofikiria, ubadilikaji wa rangi hutokana na mwanga, joto na msisimko wa neva zake kutokana na njaa au uwoga. Haihusiani na sehemu ambayo kinyonga yupo.

Katika hali ya kawaida, ngozi yake iliyo rafu (rough skin) ni ya kijani iliyochanganyika na hudhurungi iliyofifia. Katika hali ya hofu na uwoga rangi yake hubadilika na kuwa kijani iliyoiva. Hubadilika rangi hiyo kuwa hudhurungi au manjano iliyofifia katika hali ya njaa, joto la chini na jua kali.

 

Kinyonga ana rangi gani?

Kinyonga ana uwezo wa kubadilisha rangi yake haraka sana. Kiumbe huyu anaweza kuwa kijani, njano au mweupe kwa wakati mmoja na kuwa wa hudhurungi au mweusi muda unaofuata. Vilevile wanaweza kuwa na madoa. Rangi ya kinyonga hudhibitiwa na kuendeshwa na kemikali za mwilini mwake zinazojulikana kama homoni.

Wengi hudhani ya kwamba kinyonga hubadilisha rangi yake na kufanana na mazingira aliyokuwepo ili kujificha kutokana na adui zake. Hata hivyo hii si kweli, kinyonga hubadilisha rangi yake kutokana na hali ya joto au kiasi cha mwanga anachokipata, ingawa wanyama wengi hubadilisha rangi kutokana na matakwa yao.

Ngozi ya kinyonga ni angavu (transparent). Kinyonga ana seli ndani ya ngozi yake ambayo imebeba pigments (dutu za asili zinazodhibiti rangi ya tishu katika wanyama). Pale pigment ya seli fulani inapoongezeka rangi na nyingine kupungua, kinyonga hubadilika rangi kwa mfano, kama pigment za seli nyeusi zitapungua na za njano kuongezeka basi atabadilika kutoka katika weusi na kuwa wa njano.

Takriban aina 90 ya vinyonga wanajulikana. Sanasana hupatikana Afrika, Hispania, Madagascar, India na Sri Lanka.

Tofauti na mijusi wengine, kinyonga hayuko bapa na pia mkia wake ni tofauti na mijusi wengine kama vile mamba, kenge n.k. urefu wa baadhi ya mikia ya aina ya vinyonga hufikia inchi 4. Aina kubwa kabisa ya kinyonga, aliyegundulika Afrika ya Mashariki anafikia takriban urefu wa Futi mbili (60 cm).

Mkia wake unaweza kuzungushwa kama mfano wa Spring. Macho yake makubwa yanaweza kuzungushwa huku na kule kwa mwendo tofauti kila jicho au kwa kufuatana. Ana ulimi ambao una uwezo wa kukamata wadudu kwa kasi kubwa kama chakula chake.

Hizo ndizo sifa za kinyonga hasahasa katika suala la rangi yake,  kumbuka kuwa ngozi ya kinyonga ni angavu (transparent) ila rangi hutokea kwa mabadiliko ya pigment za seli.

Ikiwa una swali, maoni au ushauri jisikie huru kutuandikia. Kumbuka unaweza kushiriki katika Forum na marafiki na kuchangia mada mbalimbali kwa kujenga uhusiano mzuri baina yenu. Ahsante.

 

Category: EDUCATION | Added by: Admin (29/Jul/2013) E W
Views: 6209 | Rating: 1.9/13
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: