Home » Articles » EDUCATION

Hivi Unaifahamu Hasa Sauti Yako?

Hivi Unaifahamu Hasa Sauti Yako?

Jinsi unavyojisikia sivyo watu wanavyokusikia


Unaweza kuwa muongeaji sana, tena muigizaji mzuri tu ambaye ni chipukizi na bado hujafanya shooting hata moja kwasababu uko katika mazoezi fulani ya kuigiza, kuimba n.k.

Sasa umeshafanya video yako, umeshaimba na wakati umekaa kusikiliza unaanza kusema aaaakhh!! Inamaana hii ndiyo sauti yangu?

Ndiyo, ni bahati mbaya – na ndio kila mtu anaisikia hivyohivyo, lakini pia unaweza kujiuliza "kwanini sauti hii yangu mwenyewe leo hii siijui?”

Kumbuka kuwa sauti huingia katika masikio kwa njia kuu mbili: kwa njia ya hewa na kwa njia ya mfupa.

Sauti inayopita kwa njia ya hewa kama vile kusikiliza sauti iliyorekodiwa na mtu akiongea au kuimba, kwa mfano – inasambazwa kupitia katika ngoma ya sikio, kisha inatetemesha vifupa vitatu nyundo, fuawe na kikuku (malleus, incus and stapes)  na kisha humalizikia katika komboli (cochlea, sehemu iliyo kama spring, ina mizunguka ya nusu duara). Hii cochlea ambayo imejaa kimiminika kwa ndani, hubadilisha mitetemeko hii ya sauti kuelekea katika mfumo wa neva ambao unaenda moja kwa moja kutafsiriwa katika ubongo. Hii ndio njia ya kwanza ambayo sauti hupita.Tunachokisikia pale tunapozungumza, hii ndio njia ya pili ambayo inajulikana kama njia ya mfupa. Mitetemeko kutoka katika  koromeo la sauti pale tunapoongea huenda moja kwa moja katika komboli (Cochlea) bila ya kupitia katika sehemu zile za sauti ya nje. Fupa la kichwa yaani fuvu (Skull) hutudanganya kwani hupunguza nguvu za miteteko hii pale inaposafiri, ndio maana siku zote tunaona tukiwa na sauti tofauti pale tunaposikiliza sauti zetu wenyewe tulizozirekodi.

Mtu fulani anaposikiliza sauti yake iliyorekodiwa, ile njia ya mfupa ambayo alijua ndiyo sauti yake ya kawaida inakuwa haisikii na hivyo kuona sauti yake imebadilika na haijui na ndio sauti ambayo kila mtu anakusikia nayo ukiongea. Alisema maneno haya

Hali hii sasa inatuelewesha kwanini tusikia sauti zetu tofauti, lakini kwanini tunachukia sauti zetu? Unaweza ukaipenda sauti yako pale unapojisikia mwenyewe ukiongea lakini ukiisikia sehemu tofauti pale iliporekodiwa unaweza kuiona mbaya na kuichukia.

Hali hii inataka kufanana na ile hali ya kwamba unaweza kujipenda unapojitizama katika kioo, lakini ukaona ni tofauti na pale unapojiona katika picha uliyopiga, iwe ni video au ya kawaida tu.

Tumekua tukijipenda na kujishangaa sana pale tunapojiangalia kwenye kioo huku tukichana nywele zetu vizuri, tukijipamba kwa mapozi yote, lakini tunapoangalia picha zetu baada ya kujipiga sasa unaona hayo yote uliyoyaangalia katika kioo hayafanani kabisa tofauti na akili zetu zilivyotarajia. Hivyo tunachukia.

Hivyo fahamu ya kwamba, tunaishi siku zote tukiongea hali ya kuwa sauti zetu wenyewe hupitia katika mfumo wa mfupa na sio hewa na ndio maana sauti hubadilika pale unapoisikia kutoka nje. Hivyo endapo unahitaji kuijua sauti yako halisi basi irekodi sehemu kama vile katika redio, kompyuta au hata simu zenye sound recorder hapo ndio utaijua sauti yako halisi ambayo kila mtu anasikia hivyo.

"Hatusikii sauti zetu tunapoongea kama vile wengine wanavyoisikia, hivyo hushangazwa sana pale tunapoisikia sauti iliyorekodiwa” alisema maneno haya Pascal Belin, profesa wa saikolojia katika chuo cha Glasgow ambaye utafiti wake uliegemea katika utambuzi wa sauti. "tunakuwa wagumu kuamini kama kweli ni sauti zetu”

kwa maswali, maoni na ushauri. Jisikie huru kutuandikia katika kisanduku hapo chini. Ahsante.

Category: EDUCATION | Added by: Admin (21/May/2013)
Views: 742 | Tags: fahamu, penda, sikia, sikio, sauti | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: