Home » Articles » COMPUTER

TOFAUTI YA INBOX NA SPAM/JUNK KATIKA EMAILS NA JINSI YA KUZITUMIA


TOFAUTI YA INBOX NA SPAM/JUNK KATIKA EMAILS NA JINSI YA KUZITUMIA


Asilimia kubwa tunaotumia internet tumefungua email (barua pepe), isipokuwa kwa wachache tu ndio hawana email. Kuwa na email ni sawa na kuwa na namba ya simu kisha ukaitumia kwa mawasiliano, email hutusaidia katika shughuli nyingi sana na kubwa tunazozifanya kwa njia ya mtandao wa internet kama vile kutuma na kupokea ujumbe, ujumbe huu unaweza kuwa umeambatanishwa na faili kama vile picha, sauti, video n.k ingawa unaruhusiwa kutuma faili lisilozidi megabyte 25 kwa kila message unayotuma.

 

Katika makala hii nimepanga kuzungumzia hasa upokeaji wa email kutoka katika vyanzo au emails tofauti. Kama nilivyozungumza hapo mwanzo kuwa email haina tofauti na kuwa na namba ya simu kisha ukaitumia katika kutumiana ujumbe, katika email kuna mafaili yapatayo kama matano hivi, huenda yakazidi kutokana na aina ya email unayotumia, lakini haya matano ni lazima uyakute humu. Tuangalie faili moja moja na kazi yake kwa ufupi:-

 

 

INBOX

Hili hutumika kuhifadhi message zote ulizopokea kutoka katika emails au website tofauti, ni sawa na kwenye simu yako ya mkononi ukifungua sehemu ya message hili faili lazima utalikuta, hivyo  hili sio geni kabisa na kila mtu anajua.

 

SENTBOX

Hili hutumika kuhifadhi message zote ambazo umezituma kwenda sehemu yoyote ile, pia hili linajulikana sana na ndio maana ukilifungua faili hili utaona listi ya message zote ulizotuma na humu hazikai message zinazoingia bali zinazotoka tu.

 

DRAFT/SAVED ITEMS

Unaweza ukaandika message halafu ukataka usiitume kwanza, labda ulitaka baadae uendelee kuihariri (edit) au huna email ya huyo unaetaka kumtumia, au kwa sababu yoyote ile inayokuzuia wewe usiitume, basi kuna chaguo la kuihifadhi kwa matumizi ya baadae, hivyo ukiihifadhi message hii inaenda kukaa katika faili hili. Faili hili hukaa message zote ulizozihifadhi kabla ya kuzituma.

 

SPAM / JUNK

Kwa wote wanaotumia yahoo au Gmail faili hili huitwa Spam, lakini kwa wanaotumia Hotmail faili hili huitwa Junk. Hili faili hukaa pia message zinazoingia kama vile za inbox ila message zinazoingia humu ni zile ambazo zinaonekana sio salama kwako, yaani zina ujumbe ambao unaonekana kuwa ni mbaya kwako au kwa utapeli, message hizi hugundulika kwa maneno yake aidha yawe katika kichwa cha habari au ndani ya ujumbe wenyewe n.k (wataalamu wamejitahidi kutengeneza maelekezo katika emails kujaribu kugundua email za aina hii ambazo zinaingia humu) pia inawezekana message ikawa ni salama kwako lakini wewe mwenyewe umeamua kuifanya kuwa si salama kwa kuichagua email hiyo kuingia ndani ya faili hili kwa mara nyingine inapotumwa kwako. Na pia wewe mwenyewe una uwezo wa kuichagua email iliyoingia humu kuifanya kwa mara nyingine ikija isiingie humu ila iingie ndani ya inbox. Vile vile inawezekana ukatumiwa email nzuri tu kwa mtu au mfanyakazi mwenzako,  lakini kutokana na maneno aliyoyaandika ndani yake likanaswa neno ambalo mtandao utalishuku kuwa si salama na kufananishwa na zile za matapeli au vinginevyo, basi email kama mojamoja huingia humu, hivyo ni juu yako kuiruhusu iingie katika inbox kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "Not Spam” kilicho juu ya ujumbe uliotumiwa.

 

Unapotumiwa email usiangalie ndani ya inbox tu, angali hata ndani ya Spam au Junk huenda ikawa imeenda humu. Watu wengi wanaweza kugombana kwa jambo dogo sana la kutokujua. Unaweza kuambiwa kuwa umetumiwa ujumbe labda wa muhimu sana unatakiwa uufanyie kazi ndani ya muda muafaka, halafu ukaangalia inbox ukakuta hakuna kitu na mara ukajikuta muda wa kazi ile uliokuwa unahitajika umekwisha hivyo kujikuta mnagombana na kulaumiana, kumbe tatizo ni kwamba email iliyotumwa imeingia ndani ya Spam na wewe hukuangalia humu. Hivyo nawashauri sana kuwa mnaangalia sehemu zote yaani Inbox na Spam/Junk kwaajili ya kufahamu email mpya zilizoingia. Na sio kuangalia ndani ya Inbox peke yake.

 

TRASH/DELETED

Faili hili hukaa message zote ulizozifuta, kwa wanaotumia Yahoo na Gmail Faili hili huitwa TRASH, lakini kwa wanaotumia Hotmail faili hili Huitwa DELETED.

 

Natumaini umepata kile kilicho bora, kama una swali au jambo lolote lile kuhusiana na makala hii jisikie huru kutoa maoni yako kwa faida ya wote wanaotembelea makala hii.

 

 

Category: COMPUTER | Added by: Admin (23/Mar/2013)
Views: 826 | Tags: tofauti, Deleted, mafaili, Inbox, Spam, trash, Hotmail, Yahoo, gmail | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: