Home » Articles » COMPUTER

TOFAUTI KATI YA WEBSITE NA BLOG

TOFAUTI KATI YA WEBSITE NA BLOG

 

Tofauti kati ya Blog na Website imekuwa ikichanganya sana hasahasa kipindi hiki ambacho utasikia sana neno Blog. Lakini je umeshawahi kujiuliza kuna tofauti gani kati ya website na blog?

 

Kwa kifupi ni kwamba blog ni aina ya website ambayo inajulikana kama Web Log na kuchukuliwa herufi ya mwisho ya Web ambayo ni "b” na kuunganishwa na neno zima la mwisho ambalo ni Log na kuwa Blog. Unaweza kuwa umeshawahi kusikia kuhusu Static and Dynamic websites.

 

Blog inaweza kuwa ndani ya website au inaweza pia kujitegemea yenyewe kama yenyewe. Ikiwa una website basi unaweza ndani yake ukaongeza blog. Na blog haiwezi kabisa kuwa website.

 

Kutokana na Wikipedia, Blog ni sehemu ya website ambayo ina taarifa zenye kuongezwa na kubadilishwa kila siku huku kukiwa na nafasi ya watembeleaji kuweka maoni yao juu ya mada unazoandika humo.

 

Blog huwa mara nyingi zina taarifa nyingi mbalimbali na huwa mpya (up to date) kila siku kwani mwenye blog anakuwa akiongeza taarifa kila siku au kwa muda maalum. Na lugha inayotumika sanasana inakuwa ni rahisi na yenye kueleweka na pia taarifa zake ni rahisi kuzitafuta kwani huonekana katika Blog Achieve.

 

Katika Blog kuna kitu kinaitwa vipachiko (Posts). Kila post ina page yake inayojitegemea Lakini page kuu (main/ home page) ya blog inakuwa ina muhtasari wa mada za karibuni za Blog hiyo na kila mwisho wa mukhtasari utaona neno Read More ambapo ukibofya hapo ndiyo inakupeleka katika ukurasa maalum wa mada hiyo peke yake.

Kitu kingine ni kwamba, katika blog huhitaji kutengeneza ukurasa kwaajili ya mada unayotaka kuanzisha bali kurasa hujitengeneza automatically pale tu unapoandika mada mpya na kuisave, Lakini katika website ukitaka kuanzisha mada inabidi kwanza utengeneze page yake kisha ndiyo uandike mada hiyo.

 

Kutokana na ugumu huo ikiwa una website na unajua kwamba utahitaji kuwa na mada nyingi za kuongeza kila muda basi ni vema ukaongeza Blog katika hiyo website ili ikurahisishie kazi hiyo.

 

Mara nyingi website zinakuwa hazina taarifa nyingi sana na ndio maana nyingi zinakuwa hazina Blog ndani yake, mfano wa website ambazo hazihitaji blog ni kama vile website za vyuo, mashule, n.k kwani hakuna cha kuongeza kila siku zaidi ya kurasa maalum tu ambazo zinakuelekeza jinsi ya kujiunga na chuo fulani, uongozi wao, maabara, maktaba, ukurasa wa mawasiliano na kuhusu wao basi. Lakini website zinazokuwa na blog ni kama za habari, tuition, na mafunzo mbalimbali kwani utahitaji kila muda kuweka habari mpya au somo jipya.

 

Mara nyingi website taarifa zake zinakuwa ni zilezile tu au hubadilika mara chache sana na kama kuna jambo la kuongezeka basi hutokea kwa nadra sana au kwa kipindi maalumu.

Zifuatazo ni baadhi ya sifa za blog

 

  1. Ina sehemu ya kuacha maoni katika kila mada
  2. Inawekewa mada mpya mara kwa mara
  3. Search Engine kama vile google huitembelea mara kwa mara (Frequently crawled by Search engines) ili ijue mada mpya ulizoweka ili iweze kuziweka katika results zake pale mtu anapotafuta katika Google.
  4. Huwa na taarifa nyingi sana.

 

Kwa upande wangu ni hayo tu, unaweza kuacha maoni yako hapa ikiwa una lolote la kuongeza.


Category: COMPUTER | Added by: Admin (27/Jul/2013) E W
Views: 1610 | Tags: website, kati, tofauti, blog | Rating: 1.0/1
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: