Home » Articles » COMPUTER

JINSI YA KUFANYA WINDOWS YAKO IWAKE KWA HARAKA.

JINSI YA KUFANYA WINDOWS YAKO IWAKE KWA HARAKA.

Kwa watumiaji wa Windows XP tu.

 

Fungua Notepad (start >> all programs >> accessories >> notepad) kisha andika maneno haya ndani ya notepad  "del c:\windows\prefetch\ntosboot-*.* /q bila kuweka hizo funga semi na fungua semi. Baada ya hapo save as ntosboot.bat na hakikisha chumba cha chini cha save as type umeweka all files na hakikisha unaisave katika local disk C. angalia picha hapo chini.

 


Baada ya hapo nenda start halafu tafuta neno Run au kwa kifupi bofya katika keyboard yako alama ya windows halafu kabla ya kuiachia bofya na herufi "R” baada ya hapo Run itatokea. Kisha andika maneno haya ndani yake "gpedit.msc” usiweke hizo funga semi na fungua semi kisha bofya neno ok au bofya enter kwenye keyboard.


Window itakayotokea utatafuta neno "Windows Settings” kisha utaclick hapo mara moja. Baada ya hapo kwa upande wa kulia uta double click neno Script (StartUp/ShutDown) kisha katika maneno mawili yatakayotokea utaDouble Click ShutDown. Hapa kuna window nyingine itatokea ndogo hivi, bofya button iliyoandikwa Add… (angali picha hapo chini)

 

   

Kisha itatokea tena sehemu itakayokwambia add script… katika chumba cha Script name utabofya mbele yake button iliyoandikwa Browse… kisha utaenda kulitafuta lile faili ulilolisave hapo mwanzo katika local disk C ambalo ulilipa jina la ntosboot.bat kisha utaliselect halafu utabofya neno Open. Baada ya hapo utabofya tena ok katika windows yako ya add Script kisha itajifunga, halafu itabakia window ya Shutdown Properties ambayo nayo pia utaclick Apply halafu utaclick tena Ok kisha itajifunga. Funga kila kitu sasa twende kwenye hatua ya mwisho.

 


nenda start halafu tafuta neno Run au kwa kifupi bofya katika keyboard yako alama ya windows halafu kabla ya kuiachia bofya na herufi "R” baada ya hapo Run itatokea. Kisha andika maneno haya ndani yake "devmgmt.msc” usiweke hizo funga semi na fungua semi kisha bofya neno ok au bofya Enter kwenye keyboard.

 

Katika window itakayotokea Double click kwenye "IDE ATA/ATAPI controllers” kisha Right click kwenye neno "Primary IDE Channel" halafu click  "Properties”.Katika windows itakayotokea nenda kwenye sehemu inayoitwa "Advanced Settings" inapatikana kwa juu. Baada ya hapo kuna sehemu utaona za Device 0 na Device 1 hapa tafuta ile sehemu ya Device ambayo katika upande wa Device Type iko free kubadilishika yaani haijafungwa. Angalia picha hapo chini. Kisha sehemu hii ya device type chagua neno "None” badala ya neno Auto Detect. Kisha weka Ok.

 

 halafu tena Right click kwenye neno "Secondary IDE Channel" halafu click  "Properties”. Kisha fuata hatua zilezile ulizofanya katika Primary IDE Channel. Kisha weka OK halafu izime na uiwashe tena Kompyuta yako.

 

Hapo itawaka haraka sasa.

 

Ikiwa una swali lolote juu ya mada hii jisikie huru kuandika katika maoni yako na kama unaswali lolote Jisikie huru kutuliza hapa  Nakutakia kila la kheri.

Category: COMPUTER | Added by: Admin (28/Mar/2013)
Views: 698 | Tags: Restart, Windows, settings, right click, boot, IDE ATA/ATAPI controllers, ShutDown, Fast, add script | Rating: 1.0/1
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: