Home » Articles » COMPUTER

Hatua Rahisi Za Kufuata ili Utengeneze Website Yenye Mafanikio

Hatua Rahisi Za Kufuata ili Utengeneze Website Yenye Mafanikio


Kutengeneza tovuti nzuri ni sehemu muhimu katika kuifanya iwe na watembeleaji wengi. Imekuwa ni vigumu watu kufahamu jinsi gani watengeneze tovuti zinazoweza kuwa nzuri na vigezo vinavyovutia na kuenda na wakati. Sasa uko katika njia nzuri ya kukuelewesha suala hili. Makala hii inakupa dondoo safi kabisa kuhusu utengenezaji wa tovuti.

 

Kikubwa ni vema ukajua kwanza jina la tovuti yako kwani unaweza kutengeneza kisha ukataka kuipa jina ambalo tayari mwingine amekwishalitumia. Angalia katika search engine kama vile google au katika zile website zinazouza Domain names uone kama jina hilo bado halijapata mtu wa kulitumia.

 

Kuna windows ndogondogo zinatabia ya kujitokeza, aidha katika kona au juu au chini wakati mtu anatembelea tovuti fulani (pop – ups windows), hali hii huwakera watembeleaji wengi sana kwani inakuwa kama usumbufu kwao na kuwafanya wakose umakini juu ya kile wanachokitafuta au kukisoma katika tovuti. Browser nyingi hujitahidi kuzizuia hizi, kabla watembeleaji hawajaziona. Kwa hali hiyo jitahidi sana uepukane nazo. Kama utataka kuzitumia basi inabidi uwe umepata ushauri wa kina na kufikiria mara mbili juu ya suala zima la kuzitumia hizi.

Jaribu kudhibiti matangazo katika tovuti yako. Unapokuwa na matangazo mengi sana katika tovuti yako husababisha ikose uaminifu na kutoonekana ya kisasa. Na vilevile jitahidi matangazo yako yaendane na mada za tovuti yako.

Weka huduma ya watu kuhitaji kupokea taarifa zako kwa njia ya email (Subscribe to a newsletter). Hii itasaidia watu kufahamu kila kinachoendelea katika tovuti yako pale unapoandika au kuweka makala mpya, inasadia kuifanya tovuti yako iwe up to date.

Weka ukurasa wa "Kuhusu Sisi” (About Us), itasaidia wasomaji kujua wewe ni nani na unafanya nini. Acha watembeleaji wako wakufahamu, wajue kazi yako katika tovuti yako na mambo ya msingi kuhusiana na wewe.

Ni vizuri kuhakikisha unaweka njia ya mawasiliano au ukurasa maalum ili watembeleaji wako waweze kuwasiliana nawe pale watakapohitaji. Hata hivyo hii inaonyesha uaminifu kwa kuweka njia zako za mawasiliano wazi kwani tovuti nyingi hukosa hili na hivyo kuonekana kama wababaishaji.

Ni vema kuijaribu tovuti yako katika browser mbalimbali kwani kila browser inaweza kuonyesha tovuti yako kwa njia tofauti hivyo ni vema ujue tofauti hizo na ujue ni jinsi gani ya kuzirekebisha. Inawezekana ukaona tovuti yako vizuri kwenye Internet Explorer lakini ikaonekana vibaya katika Mozilla Firefox au Google Chrome au Safari.

 

Tovuti nzuri ni ile ambayo ni rahisi kufunguka, hivyo basi, jitahidi uepukane au upunguze vile vitu vinavyosababisha tovuti kufunguka haraka kama vile kuweka Flash Animations nyingi katika tovuti, kuweka picha zenye saizi kubwa katika tovuti n.k.

Tovuti nzuri inapaswa kutengenezwa na kupangiliwa vizuri kwa kuhakikisha urahisi wa mtu kutafuta kile anachokihitaji. Kwa kuweka au kuipangilia hovyo huweza kuwafukuza watu wasirudi tena kuisoma kwani kila wanapoingia humo hawaoni mwanzo wala mwisho.

Pia ijulikane kuwa huwezi kwa pekeyako kutengeneza tovuti kisha ukaipitisha mwenyewe na kuiweka hewani bila kumshirikisha mtu yeyote kwa ushauri. Inapendeza na inaleta mafanikio endapo utahitaji msaada wa hapa na pale na ushauri kutoka sehemu na wataalamu mbalimbali.

Ifanye tovuti yako iwe ya kirafiki zaidi kwa kuwapa uhuru watembeleaji wako kutoa maoni kuhusiana na kile tovuti yako inachokionyesha ili uelewe matatizo yako madogomadogo na kuyarekebishe ili uepushe hali ya kuwakimbiza watembeleaji na wateja wako. Na jitahidi kujibu matatizo yao kwako wanapokuandikia.

 

Usikate tamaa kwa kukosolewa bali mshukuru sana anayekukosoa kwani ndio njia sahihi ya kufanya kile kilicho bora zaidi.

 


 

Category: COMPUTER | Added by: Admin (31/May/2013)
Views: 685 | Tags: dondoo, website, mafanikio, tengeneza, hatua, fikra, tovuti, maendeleo | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: