[ New messages · Members · Forum rules · Search · RSS ]
  • Page 1 of 1
  • 1
Forum » EDUCATION » GENERAL EDUCATION » FAHAMU UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU
FAHAMU UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU
AdminDate: Sunday, 13/Oct/2013, 17:09 | Message # 1
Sergeant
Messages: 30
Awards: 5
Reputation: 1
Status: Offline

                                           FAHAMU UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU


Unaweza kuwa umeshawahi kusikia neno SAIKOLOJIA mara nyingi sana, Lakini
hebu tufafanue zaidi kwa yule ambaye hafahamu maana yake. Kwa kifupi
kwanza hili neno ambalo asili yake ni kigiriki likiwa na maana ya
kwamba, saiko ni mambo yanayohusu akili au ubongo, na lojia ni mambo
yanayohusu elimu. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kwamba saikolojia ni
elimu inayohusu mambo ya akili au ubongo.

Somo hili la saikolojia linahusu jinsi wanyama na binadamu wanavyoweza
kutumia akili au ubongo katika kumiliki na kuongoza vitendo na tabia
zao.

Ni wazi kuwa wanyama wote wana ubongo Lakini ni binadamu peke yake ndiye
mwenye uwezo wa kujifunza kwa kutumia ubongo wake wakati wanyama
wengine hujifunza kwa kutumia silika na mazoea. Na hii humfanya binadamu
kuwa tofauti na viumbe wengine.

Sehemu kubwa ya saikolojia inahusu jinsi binadamu anavyoweza kutumia
ubongo au akili yake katika kujifunza, kufikiri na kudhibiti tabia zake.

Kwa ujumla ni kwamba saikolojia ni taaluma ya kisayansi inayohusu
tabia/mienendo na michakato ya ubongo au akili ya binadamu katika
kujifunza. Tabia au mienendo ni kila kitu ambacho mtu hufanya na ambacho
huweza kuchunguzwa moja kwa moja.

Tumeangalia kwa ufupi sana maana halisi ya saikolojia, sasa je unaelewa nini kuhusu saikolojia ya elimu?

Kuna matawi mbalimbali ya saikolojia kama vile saikolojia ya Elimu,
Saikolojia ya Kliniki, saikolojia ya Biashara, saikolojia ya Kijeshi
n.k. hivyo basi katika mada hii tunaangalia maana ya saikolojia ya elimu
na umuhimu wake.

Saikolojia ya elimu ni tawi la taaluma ya saikolojia linaloshughulikia masuala ya elimu, tawi hili linachunguza jinsi mwanafunzi anavyojifunza
mambo mbalimbali ya kielimu, kijamii na kiutamaduni na namna bora ya
kumfundisha. Sasa hebu tuangalie tawi hili lina umuhimu gani? Au kuna
umuhimu gani wa mwalimu kujua saikolojia?

Read more at: http://staryte.com/publ....1-0-226

Copyright © Staryte Pro
Attachments: 8998183.png(72.3 Kb)
 
Forum » EDUCATION » GENERAL EDUCATION » FAHAMU UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU
  • Page 1 of 1
  • 1
Search: