Home » 2017 » September » 9 » Alibaba na wezi 40 Part 1
14:44
Alibaba na wezi 40 Part 1

ALIBABA NA WEZI 40

 

SURA YA KWANZA:

HAZINA KATIKA PANGO

Hapo zamani za kale katika mji wa persia waliishi ndugu wawili mmoja aliitwa Kasim na mwengine aliitwa Alibaba, ndugu hawa wawili walikuwa na baba yao ambae alikuwa na uwezo wa kifedha kidogo ambae alipokufa waligawana mali zake mgao sawa kwa sawa bila kumzidishia yeyote baina yao, na wala hawakuwa na muda wa kupoteza na kuzitumia mali zile zote. Mkubwa kati ya wale vijana wawili ambaye ni Kasim alioa mwanamke ambae ni mtoto wa mfanya biashara tajiri, hivyo basi, baba mkwe wake alipotangulia mbele ya haki (kufa) alimiliki duka kubwa lililokuwa na bidhaa adimu pamoja na bidhaa zenye thamani kubwa na pia alimiliki bohari kubwa iliyokuwa na vyombo vyenye thamani kubwa ukiachilia mbali dhahabu nyingi sana ambazo zilikuwa zimefukiwa ardhini. Hivyo basi alijulikana karibuni mji mzima kama mtu aliye thabiti au imara mwenye nguvu lakini mke aliyemuoa Alibaba alikuwa masikini na tegemezi hata hivyo waliishi katika kibanda duni. Alibaba alijikimu maisha yake kwa kuuza kuni alizokuwa akikusanya kutoka msituni na kupeleka mjini sokoni kwa kutumia punda wake watatu.

 

Ilitokea siku moja Alibaba alikuwa akikata matawi yaliyokufa na kukausha kuni zilizotosheleza kwa mahitaji yake, na baada ya hapo akaweka mizigo yake juu ya wale wanyama wake (punda). Mara ghafla akaona kama wingu la vumbi likiwa linapanda juu angani kwa mbali upande wake wa kulia huku likiwa linakuja upande alioko, lilipofika karibu aliona kundi la waendesha farasi wakiwa wanakuja upande alioko na walikuwa karibuni kumfikia. Kwa muda huo alikuwa kakata tamaa na kuogopa huenda wale wakawa ni majambazi ambao wanaweza kumuua na kuchukua punda wake, kwa uwoga wake akaanza kukimbia. Lakini kwakuwa walikuwa tayari wamefika karibu na hakuweza kutoka nje ya ule msitu, aliwaficha wanyama wake  vichakani naye kujificha kwenye mti mkubwa ambapo alikaa kwenye tawi ili aweze kuona kila kinachoendelea pale na wakati huo hakuna yeyote chini aliyeweza kumuona huko juu aliko. mti ule uliota pembeni kidogo ya mwamba ambao ulikuwa mrefu.

 

Waendesha farasi, vijana, wenyenguvu na mashujaa walikuja karibu na uso wa ule mwamba na wote wakashuka kwenye farasi wao kitendo ambacho kilifanya Alibaba awaone vizuri watu wale na mara akapata hisia kutokana na muonekano na mwenendo wa tabia za wale watu kwa jinsi alivyowaona ni waporaji ambao wamepora na sasa wameleta mali za uporaji kuja kuziweka katika eneo lile kwa nia ya kuzificha, vilevile aligundua kuwa idadi ya wale watu ilikuwa arobaini (40). Alibaba aliwaona wale majambazi na walipofika chini ya ule mti kila mmoja alimfunga farasi wake pale, halafu kila mmoja alishusha mizigo yake ambayo Alibaba aligundua kuwa kulikuwa na madini ya dhahabu na fedha ndani yake. Mtu mmoja kati yao ambae alionekana kuwa ndiye kiongozi wao aliendelea mbele huku akiwa na mzigo kwenye bega akipita kwenye mibamiba na vichaka mpaka alipofika sehemu moja kwenye alama chini kama doa hivi akasimama pale halafu akatamka maneno fulani akisema “Funguaaaaa, Sesmiii!!” na mara moja ukafunguka mlango mkubwa kwenye uso wa ule mwamba, baada ya hapo wezi wote wakaingia mle ndani na mwisho akaingia kiongozi wao kisha lile lango likajifunga lenyewe.

Muda mrefu walikaa ndani ya lile pango huku Alibaba akiendelea kukaa juu ya ule mti akihofu kwamba kama akishuka huenda mude uleule na wale wezi wanaweza kutoka na kumuona kisha wakamuua. Lile lango lilipofunguka tu wa kwanza kutoka alikuwa ni kiongozi wao akaenda kwenye lile doa kisha akawahesabu wale wenzake mpaka walipoisha kutoka wote kisha akasema “Fungaaaaaaa, Sesmiiii!!” na hapo lango likajifunga. Walipomaliza kukutana wote kila mmoja alichukua mizigo yake na kuondoka wote eneo lile wakiongozwa na kiongozi wao wakielekea kule walikotokea. Alibaba aliendelea kukaa juu ya ule mti huku akiangalia safari ya wale wezi wanapoondoka. Akaona asubiri mpaka wapotee kabisa kwa maana asije mmoja akarudi na kumkuta mahali pale.

 

Walipopotea kabisa mbele ya macho yake Alibaba akashuka kutoka mtini na kwenda mpaka pale kwenye lile doa kisha akajisemea mwenyewe “nitajaribu kutamka maneno yale ya ajabu nione kama kwa kutamka kwangu lile lango litafunguka na kufunga” kisha akasema kwa kelele yale maneno “Funguka, Sesame!!” alipomaliza tu kutamka mara lango likafunguka, kisha akaingia ndani yake.

Akaona pango kubwa lenye kuba likiwa na urefu upatao kadiri ya urefu wa mtu aliekuwa mrefu zaidi duniani, pango lile lilikuwa limezungukwa na mawe na lilikuwa likipitisha mwanga kupitia vitundu vidogovidogo vilivyokuwa katika pango lile na kushangazwa alipoona limejaa kila aina ya bidhaa mle ndani na kumerundikwa kutoka chini mpaka juu rundo la mizigo ya hariri na nguo nzuri zilizotiwa nakshi na matuta juu ya matuta ya makapet na mazulia yenye rangi tofauti na pia aliona sarafu za dhahabu na fedha zikiwa nyingine zimezagaa chini na nyingine zikiwa ndani ya mifuko. Kwa kuona wingi wa mali hizi Alibaba alijifikiria moyoni kuwa sio kwa miaka michache tu, hii itakuwa ni karne na karne wezi wanapora mali za watu na kuja kuzificha humu. Je nini kitaendelea humo pangoni? Usikose kisa hiki wiki ijayo

*****END *****

endelea sehemu ya pili

Category: Stories & Entertainment | Views: 205 | Added by: Admin | Rating: 1.0/1
Total comments: 5
4  
Moh vp mbona dry

2  
Hii story nimeipenda sir Fanya utuekee part 2  plzzzzzz

0
3  
Usijali iko njiani Part 2

5  
Adminnnnn. Anna part4

1  
The best story ever

Name *:
Email *:
Code *: